MBINU YA KUWA NA WATEJA WENGI

Wajasiliamali na wafanya biashara wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi kufikilia ni kitu gani afanye ili ajipatie WATEJA wakutosha kusudi mtaji wake ukue haraka na ajipatie mafanikio mazuri ya kiuchumi.

Zifuatazo ni mbinu 20 ambazo ukizifahamu na kuzingatia vyema utakuwa na WATEJA wengi katika biashara yako , lakini kwa leo tutajifunza mbinu 10.

1. Kukidhi mahitaji ya mteja. Mteja anapenda afike dukani kwako au katika ofisi yako apate kile anachokitafuta ili asijione amepoteza muda wake kuja kwako na akikosa siku hiyo atajenga taswira ya kuamini ya kuwa huwa hauuzi BIDHAA anazotaka. Hivyo jitahidi kuwa na ile BIDHAA ambayo mteja anaitafuta.

2.kuwa mbunifu. Mfanyabiashara unapaswa kuwa mtu ambaye unafikilia kufanya kitu ambacho hakipo katika mazingira unayoishi eidha kwa kuleta bidhaa mpya au ya zamani huo ni ubunifu, kubuni muundo wa uendeshaji wa biashara mzuri na mwepesi kwa wateja wako, na kuboresha ofisi yako na usafi binafsi na mazingira pia.

3.kuwa na lugha nzuri . Zipo kauli ambazo unatakiwa kumjibu mteja wako hata kama amekuuzi namna gani kwani na yeye Ni mwanadamu ambaye anaweza kukosea kumbuka kabisa wahenga walisema “mteja ni mfalme” anapaswa kutunzwa na kuhudumiwa vizuri kwani ukifanya hivyo wateja huwa wanajiskia vzuri na kukufanya wewe kuwa rafiki yao.

4.uza bidhaa zenye ubora. Achana na bidhaa fake na zilizo na bei ndogo eti kisa una bana mahemezi , mambo haya huwa yanawafanya wateja wasikuamini na kuona ya kuwa unabidhaa mbaya kwahio kurudi kwako sio rahisi na wataambiana wengi utajikuta unapoteza hadi wateja wa awali na kuomba usifanye ivo.

5. kuwa muaminifu. Hautakiwi kuwa na tabia mbaya za kuwa unadhuluma hela na bidhaa unazo kopeshwa na kuachiwa na WATEJA wako kuwa mtu mkweli na muwazi utakuwa na wateja wengi na wakudumu .

6.Fanya matangazo ya kibiashara. 4 m3uu wendo wa kuwajulisha wateja juu ya biashara yako unanini kipya?, unajihusisha na nini?bei zako zipoje? Offer,n.k fanya matangazo ya mtandaoni, andika mabango, vyombo vya habari,n.k.

7.kuwepo muda wote kazini. Jitahidi uwepo eneo la kazi kwa muda unaotakiwa kwani unapokuwepo wateja wataamini ya kuwa wewe huwa haukosi kazini hivyo wengi watakuwa na uhakika was kupata huduma endapo wakija kwani haitakuwa na maana mteja anakuja anakuta pamefungwa inauudhi na kuchosha pia even you lazima uchoke.

8. Zingatia utoaji wa elimu na ushauri. Elimu unayotoa kwa mteja pamoja na ushauri Ina nguvu kubwa sana ya kufanya uaminike kwao na kutegemewa hasa kwa Yale wasio ya just ,waambia ubora wa bidhaa yako na madhara , faida na hasara ya kitu .

9.jifunze saikolojia ya wateja . Jambo hili ni msingi wa mfanya baishara ambapo anatakiwa atambue mambo yafuatayo ya kisaikolojia furaha,huzuni,utani, hasira na tabia yakr kiujumla kwani utakapoyajua haya utakuwa meepesi kumjibu mteja wako majibu mazuri kwa maswali utakayoulizwa na yeye atasifia utoaji wako wa huduma.

10.Jenga tabia ya kumuomba MUNGU. Anaetoa kibari Ni Mungu peke yake muuombe akupe watu kwani unaweza kufanya Kila namna ili upate upate wateja wengi ila kama Mungu asipotaka bado itakuwa ngumu kwako .

Hizi Ni mbinu ambazo Mimi nimetumia ili kujipatai wateja wengi na wakudumu pia makampuni ,wajasiriamali, na wafanyabiashara wakubwa wamezitumia. Ahsante kwa kujifunza zaidi , ombi langu kwako weka comment yako juu ya makala haya ili nijue ni kipi kinatakiwa tena . Wako. Na mfanyabiashara Filbert Jonathan lunigangwa.

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started