Habari !. Leo tutajifunza njia kuu tatu za kuanzisha biashara . Kabla kufungua ofisi yako ya kibiashara au ya kijasiliamali nilazima kuzingatia mambo haya 3 ili ukuwe kimaendeleo kwa halaka sana na isivyo kawaida kwa watu wengine. NJIA 3 ZA KIJASILIAMALI NA KIBIASHARA. (1) BIDHAA. BIDHAA ni kitu ambacho unatakiwa kufikilia kabla hujawa na mtaji Wala na kitu kingine kile , bidhaa nzuri Ni ile ambayo inaonekana Ina umuhimu mkubwa katika jamii inayokuzunguka au jamii za watu , mfano ziko biashara ukizianzisha Ni lazima utafanya vizuri Kama vile ya madawa ya binadamu, mahitaji ya Kila siku Kama chumvi,sabuni,mafuta ya Petro na ya Kila n.k (2)ENEO LA KIBIASHARA(SITE) Tafuta eneo zuri lenye muonekano wa kufaa kwa bidhaa/huduma unayotamani kuifanya kwani yapo mazingira ambayo ukipeleka bidhaa fulani inashindwa kuuzika mfano eneo la joto upeleke nguo za joto kama jaketi,blanketi,makoti mazito,n.k.vitu hivi vitafaa sana Kama ukipeleka maeneo ya baridi mfano mbeya ,Lindi na sehemu zingine, hivyo unatakiwa kujua mambo haya kabla ya kwamba ziko biashara za kijijini tu au mjini usikulupuke . (3)LENGO. Lengo hili Ni wazo au kusudi litakalokufanya uwanzishe mradi wako , na dhumuni kubwa la kuwa na malengo Ni kukupa nidhamu ya pesa , moyo wa kutokukata tamaa, kujituma kwa bidii , kuipenda biashara yako na hii Ni kwa sababu utakuwa na vitu unatamani uvipate katika maisha yako. Ahsante!!! ENDELEA KUFATILIA BLOG HII KWA MASOMO YA KIBIASHARA